Biden na XI waahidi kuimarisha uhusiano na mawasiliano kati ya nchi zao

Rais Joe Biden akimkaribisha mgeni wake Xi Jingping katika bustani ya Filoli

Rais Joe Biden na Rais Xi Jinping wa China wamekubaliana kuanza tena mawasiliano ya moja kwa moja kati ya maafisa wanadamizi wa jeshi walipokutana kwa mara ya kwanza kwa mkutano wa kilele baada yam waka mmoja Jumatano.

Viongozi hao wawili wanasema walikua na mazungumzo yaliyokuwa na maana nay a dhati, na kutembea pamoja katika bustani ya kihistoria ya Filoli nje ya mji wa San Fransico wakati wa mazungumzo yao ya saa nne. .

Akizungumza na waandishi habari baada ya mazungumzo yao kabla ya kuanza mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Kiuchumi ya nchi za Asia na Pasifik APEC, Rais Biden amesema wamekubaliana kuanza tena kwa misingi ya usawa na heshima mawasiliano ya moja kwa moja kati ya maafisa waandamizi wa kijeshi, na wamekubaliana pia kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja kati yao wakati wa mzozo wowote ule.

Rais Joe Biden na Rais Xi Jingping wakitembea kwenye bustani ya Filoli, mjini Woodside.

Biden amesema mafanikio makubwa kwenye mazungumzo hayo ni Xi kukubali kushirikiana katika vita dhidi ya dawa za kulevya akikubali kupunguza uzalishaji wa dawa hatari ya fentanyal nchini mwake, inayodaiwa kua sababu ya janga la utumiaji dawa za kulevya na maafa nchini Marekani.

Lakini Xi na Biden wangali wanatafautiana juu ya suala la kisiwa cha Taiwan, ambapo rais wa China alimwambia mweneyji wake kuacha kukipatia kisiwa hicho silaha na kwamba mungano ni jambo "lisiloweza kuzuilika."

Viongozi hao wawili hawajakutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana tangu mazungumzo ya Bali Novemba 22, na tangu wakati huo uhusiano ulianza kuyumba baada ya Marekani kutengua puto la Uchina iliyodaia ni chombo cha upelelezi.

Wakati wa mazungumzo yao Xi amesema uhusiano kati ya Marekani na Uchina, ambao ni uhusiano muhimu kabisa kati ya mataifa mawili duniani, unabidi kuendelea kwa njia ambayo itanufaishia wakazi wa nchi zote mbili na kukidhi wajibu wao katika maendeleo ya binadamu.