Matukio ya siku ya 7 tangu kuanza mapigano kati ya Israel na Palestina
Wafuasi wa chama cha kisiasa na kidini cha Pakistan cha Jamaat-e-Islami wahudhuria maandamano dhidi ya mashambulio ya anga ya Israel huko Gaza, na kuwaunga mkono wa Palestina mjini Karachi, Pakistan. Jumapili Oct 15, 2023.
Waandamanaji wakibeba mabango yenye maandishi yanayounga mkono watu wa Palestina katika mji mkuu wa Hispania wa Madrid. Oktoba 15, 2023.
Watu waandamana kuunga mkono watu wa Israel katika ufukwe wa Copacabana mjini Rio de Janeiro, Brazil Oktoba 15, 2023.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken azungumza na waandishi habari mjini Cairo kabla ya kuelekea Jordan, akiwa kwenye ziara ndefu ya nchi za Mashariki ya Kati kutafuta njia za kuzuia mapigano ya Gaza, kati ya Israel na Hamas.
Watoto wakipalestina wakiangalia jengo la familia ya Zanon lililobomolewa kutokana na mashambulizi ya ndege mji wa Rafah kwenye ukanda wa Gaza. Oktoba 14, 2023.
Mama wa kipalestina akibusu sanda iliyofunikwa mwili wa mtoto mdogo aliyeuliwa wakati wa shambulizi la ndege la Israel Jumapili Oktoba 15, 2023.
Moto mkubwa na moshi ukitanda hewani baada ya kudondoshwa bomu la Israel mjini Rafah, Ukanda wa Gaza October 15, 2023.
Jamaa za Wamarekani walochukuliwa mateka na Hamas wakionesha picha zao mjini Tel Aviv.
Margentina aliyejikuta kati kati ya vita kati ya Israel na Hamas akipokelewa na familia yake aliporudi nyumbani kwenye uwanja wa ndege wa Buenos Aires.
Buldoza ikiondosha vifusi kutafuta ikiwa kuna watu walofukizwa huku watu wakitizama katika mjaa mjini Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji wakipeperusha bendera ya Palestina na mabango yenye maandishi yanayoiunga mkono watu wa Palestina mjini Madrid, Oktoba 15, 2023.