Kila mmoja kati ya wagombea hao alikua anajaribu kua mpinzani mkuu wa mgombea anaeongoza kwenye uchunguzi wa maoni ya Warepublican, rais wa zamani Donald Trump.
Kiongozi huyo anaongoza kwa kiwango kikubwa kuweza kuteuliwa mgombea wa chama katika uchaguzi wa 2024, licha ya kwamba anakabiliwa na mashitaka manne ya uhalifu.
Mchambuzi wa masuala ya kisaisa Amin Mwidau anasema mdahalo ulikua na mabishano mengi na wagombea hawakuweza kueleza misimamo yao namna inavyotakiwa.
"Hatujamuona hata mmoja wao ambae amibuka juu zaidi ya mwengine isipokua kila mmoja alikua anamshambulia mwenzake, na yule ambae alionekana amefanya vizuri kwenye majadiliano yaliyopita alishambuliwa zaidi," alisema Mwidau.
Wagombea hao walitumia muda wao pia kumshambulia Trump kwa kutohudhuria mdahalo huo. Gavana wa zamani wa New Jersey Chris Christie alimshambulia akisema kwamba anakimbia kuweza kujibu mashuala nyeti yanayomkabili na ni muoga.
Turmp mwenyewe alikua na mkutano wa hadhara siku ya Jumatano huko Michigan, ambako wafanyakazi wa kutengeneza magari wa kampuni tatu kuu wanagoma kwa wiki mbili sasa.
Kwenye mdahalo wagombea wa chama cha Republican walishambuliana kwa namna haijapata kushuhudiwa katikia juhudi za kumshinda mwengine, na kama Mwidau anasema ni kujaribu kujiweka katika nafasi ya pili ili kuchukua uwongozi pindi Trump hatoweza kushindana kutokana na maswala mbali mbali pamoja na kesi zinazomkabili
Your browser doesn’t support HTML5