Waziri Mkuu wa India Narendra Modi atoa wito kwa AU kufanywa mwanachama wa G20

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akisalimiana wakati akiondoka baada ya kuhudhuria siku ya tatu ya Mkutano wa wakuu wa G20 wa siku tatu huko New Delhi Agosti 27, 2023. (Photo by Sajjad HUSSAIN / AFP)

Siku ya Jumapili mwenyeji wa sasa wa G20 Modi pia alitoa wito wa kujumuisha eneo la  Afrika nzima ambalo kwa pamoja lilikuwa na Pato la Taifa la dola trilioni 3 kwa  mwaka jana.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alitoa wito Jumapili kwa Umoja wa Afrika kufanywa kuwa mwanachama wa G20 huku pia akiitaja nchi yake kama suluhu ya matatizo ya usambazaji bidhaa kabla ya mkutano wa Umoja huo utakaofanyika mjini New Delhi mwezi ujao.

Kundi la nchi 20 zenye uchumi mkubwa duniani lina nchi 19 na Umoja wa Ulaya (EU), unaounda takriban asilimia 85 ya Pato la Taifa la dunia na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani lakini Afrika Kusini ndiyo pekee mwanachama kutoka barani Afrika.

Mwezi Desemba, Rais wa Marekani Joe Biden alisema anataka Umoja wa Afrika kujiunga na G20 kama mwanachama wa kudumu akiongeza kuwa imechukua muda mrefu kutokea lakini itafanyika.

Siku ya Jumapili mwenyeji wa sasa wa G20 Modi pia alitoa wito wa kujumuisha eneo la Afrika nzima ambalo kwa pamoja lilikuwa na Pato la Taifa la dola trilioni 3 kwa mwaka jana.