China ina wasiwasi na azimio la Marekani na Korea Kusini dhidi ya Korea Kaskazini

Azimio  la pamoja ambalo limetangazwa na Washington, na Seoul, kuongeza vizuizi vya  nyuklia dhidi ya  Korea Kaskazini limeifanya Beijing kutoa ukosoaji ambao unaonyesha mtizamo wake kuhusu  ushirika huo unatishia ushawishi katika eneo lake wataalamu wamesema.

Msemaji wa ubalozi wa China hapa Washington, Liu Pengyu ameieleza VOA kwamba China imeona maudhui muhimu kwenye azimio la Washington.

Ameongeza kusema kwamba tabia ya Marekani ni matokeo ya mtazamo wake kwa vita baridi, na kwamba kile Marekani inachokifanya kinasababisha uchokozi wa kikanda, kudhoofisha mifumo ya nyuklia isiyo na madhara, na kusumbua maslahi ya kimkakati na mataifa mengine.

Azimio la Washington ambalo rais wa Marekani, Joe Biden na rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, wamelitoa Aprili 26, linajumuisha juhudi za kukabiliana na mashambulizi ya nyuklia kutoka Korea Kaskazini.

Washirika walikubaliana kuongeza sauti ya Seoul katika mipango ya nyuklia ya Marekani kupitia chombo maalumu.