Marais wa Iran na Syria watia saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano

Marais wa Iran, na Syria, Jumatano wametia saini mfululizo wa makubaliano ya ushirikiano katika mafuta na sekta nyingine ili kuboresha uhusiano wa kiuchumi baina ya washirika hao wawili.

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, aliyengoza ujumbe mkubwa wa kiuchumi na kisiasa, alikutana na mwenzake wa Syria, Bashar Al Assad, baada ya kutua katika taifa hilo lililopo vitani kwa ajili ya ziara ya siku mbili na kuwa ziara ya kwanza kwa rais wa Iran mjini Damascus toka mwaka 2010.

Tehran imekuwa muungaji mkono mkubwa waserekali ya Assad toka kuzuka kwa vuguvugu la mwaka 2011 na kugeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kuwa kiungo muhimu katika kurejesha wimbi la mgogoro kuwa na mwelekeo wa ushindi kwake.

Iran imepeleka washauri kadhaa wa kijeshi, na maelfu na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran kutoka kote mashariki ya kati kwenda Syria kupigana upande wa Assad.