Somalia kufanya Sensa ya watu na makazi

Serikali ya Somalia imezindua sensa yake ya kwanza ya kitaifa ya watu na makazi baada ya miongo kadhaa kupita ambayo inatarajiwa kuchukua miaka miwili.

“Tutahesabu watu wanaoishi katika eneo la Somalia na nyumba wanazoishi Dk Abdi Ali Ige, mkuu wa sensa ya watu na makazi ya Somalia," aliiambia VOA Jumanne.

Ige, ambaye atasimamia mradi huo alisema wakusanyaji wa taarifa watafuata mbinu ya kawaida inayotumiwa kimataifa kuhesabu.

“Tunatumia mchanganyiko wa mbinu za kitaalamu, ambapo tunahesabu idadi ya watu tunayoipata kwa siku alisema.”

Kwa idadi ya watu wanaohamahama na wasio na makazi, amesema watutumia mbinu inayostahili ambapo watauliza watu mahali wanapoishi kwa kawaida na matumizi ya mbinu mbili yanafanyika kwa sababu Wasomali wana matabaka tofauti ya idadi ya watu.

Ige alisema sensa itaanzia kwa wakazi wa mijini kisha kuhamia vijijini kwa watu wanaohamahama.