Rais Biden kukutana na Demokrat na Republikan kushughulikia deni la taifa

USA-BIDEN/

Rais Joe Biden, wa Marekani wiki ijayo atakutana na viongozi wa vyama vya Demokrat na Republikan wa baraza la wawakilishi na Seneti.

Kikao hicho ni cha juhudi za kuepusha janga la kutolipa deni la taifa ambalo linaweza kutokea kwa muda wa mwezi mmoja.

Uwezo wa serikali ya Marekani wa kukopa fedha unakabiliwa na ukomo wa kiwango cha deni wizara ya fedha ya Marekani inaweza kupata.

Kiwango cha deni kwa sasa kimewekwa kuwa cha dola trilioni 31.4, ambayo serikali ilifikia mwezi Januari, na kulazimisha wizara ya fedha kutumia kile inachotaja kama hatua zilizo pitiliza kuendelea kulipa deni la taifa bila kushindwa.

Siku ya Jumatatu waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen alionya kwamba ilikuwa ni jambo la haraka bunge inapaswa kushughulikia ili kulinda imani kamili ya ukopaji wa Marekani na kuwakumbusha kusubiri mpaka dakika za mwisho kutaleta madhara kwa taifa.