Mlipuko mwingine wasababisha ajali ya treni Ukraine

Mlipuko ulisababisha treni ya mizigo kuacha njia kwa siku ya pili mfululizo katika eneo la Russia linalopakana na Ukraine Jumanne, na kudondosha baadhi ya mabehewa, mamlaka zilisema.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la magharibi la Bryansk, ambalo linapakana na Ukraine na Belarus.

Maafisa wa Russia wanasema makundi ya hujuma yanayoiunga mkono Ukraine yamefanya mashambulizi mengi tangu Russia ilipoivamia Ukraine mnamo Februari 2022.

“Kifaa kisichojulikana kililipuka karibu na kituo cha reli cha Snezhetskaya lakini hakuna aliyeumia,” gavana wa eneo la Bryansk Alexander Bogomaz aliandika kwenye Telegram.

Kutokana na tukio hilo kichwa na mabehewa kadhaa ya treni hiyo ya mizigo yaliacha njia, aliongeza bila kusema nani aliyehusika.