Ukraine inamalizia maandalizi ya mashambulizi ya kujibu mapigo yanayo tarajiwa dhidi ya Russia, na rais wake Volodymyr Zelenskyy anasema taifa lake litapambana bila kujali wana ndege za kivita za mataifa ya magharibi au la.
Maendeleo ya mapambano ya Ukraine yanategemea kwa kiwango kikubwa vifaa vya kijeshi kutoka mataifa ya magharibi.
Wataalamu wa kijeshi wanasema bila ndege za kivita za kisasa kutoka kwa washirika wa Kyiv wa NATO, mapambano ya kujibu mapigo kwa kiwango kikubwa yatakabiliwa na mapambano yatakayo idhoofisha.
Katika siku za hivi karibuni, katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa magharibi kufanya mkutano na uongozi wa Ukraine, na komandi ya kijeshi.
Amesisitiza kwamba kupitia mawasiliano na kundi linalo ongozwa na Marekani, washirika wa NATO na wadau wake wametoa asilimia 98 ya magari ya kivita yaliyo ahidiwa kwa Ukraine ikijumuisha 1,550 ya mashambulizi, vifaru 230, na kiwango kikubwa cha risasi.