Spika McCathy ataka Russia kujiondoa Ukraine

Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani, Kevin McCathy, Jumatatu amesema Russia lazima ijiondoe Ukraine, akikosoa vikali mauaji ya Russia ya watoto.

Hatua hiyo imekuwa ni ya kujitenga na baadhi ya Warepublikan wanaopinga msaada zaidi wa Marekani kwa Ukraine kutokana na uvamizi wa Russia.

Akiwa Israel katika ziara yake ya kwanza kama spika, McCathy amesisitiza umuhimu wa msaada kwa Ukraine, na kupinga madai kwamba haungi mkono kutuma msaada wa kifedha na kijeshi kwa Kyiv.

Katika mkutano na wanahabari, pia amesisitizia msimamo wake kuhusiana na masuala mengine ya Marekani ikijumuisha matakwa yake na mazungumzo ya kiwango cha deni la taifa na rais Joe Biden.

Akimjibu mwanahabari wa Russia, amesema kwamba ameipigia kura Ukraine na kuunga mkono misaada kwa Ukraine, na kusema haungi mkono mauaji ya Russia ya watoto na inapaswa kujiondoa Ukraine.