Waziri wa fedha wa Marekani ataka bunge kushughulikia haraka ukopo wa deni la taifa

Waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen, amelifahamisha bunge Jumatatu kwamba Marekani inatarajiwa kufikia kikomo cha deni lake mapema Juni 1 kama wabunge hawata ongeza kiwango ama kuondoa marufuku ya ukopaji ya sasa

Katika barua kwenda kwa baraza la wawakilishi na viongozi wa Senate, Yellen ametoa mwito kwa bunge kulinda imani kamili na hadhi ya ukopaji ya Marekani kwa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo kushughulikia kiwango cha ukopaji cha dola trilioni 31.4 cha kisheria cha mamlaka ya ukopaji.

Wizara ya fedha Jumatatu imesema inapanga kuongeza kiwango cha kukopa katika kipindi cha mwezi Aprili na Juni ya robo ya mwaka huu hata kama serikali kuu ipo karibu kukiuka kiwango cha ukopaji.

Marekani inapanga kukopa dola bilioni 726 katika kipindi hicho cha robo mwaka.

Hiyo ni zaidi ya dola bilioni 449 iliyo bashiriwa Januari kutokana na kiwango kidogo cha akiba cha mwanzo wa robo mwaka.