Watu wanaokabiliwa na mfumuko wa bei, na kutaka haki ya kiuchumi waliingia mitaani barani Asia, Ulaya, na Amerika Jumatatu kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani katika hali ambayo haijashuhudiwa kabla ya marufuku za dunia nzima za janga la Covid-19.
Maadhimisho yalilazimika kufanyika kutokea majumbani nchini Pakistan, kutokana na hali ya kisiasa kama ilivyo Uturuki kwa kuwa mataifa yote mawili yapo katika harakati za uchaguzi.
Vita vya Russia na Ukraine vilifunika kiwango cha shughuli jijini Moscow, ambapo sherehe hizo zilizo endeshwa kikomunisti za siku ya wafanyakazi zilikuwa ni tukio kubwa.
Kote Ufaransa baadhi ya watu 800,000 waliandamana amesema waziri wa mambo ya ndani Gerald Darmanin.
Waliandamana kupinga hatua ya karibuni ya rais Emmanuel Macron ya kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 mpaka 64.
Waandamanaji wanaona hilo ni tishio kwa haki za wafanyakazi huku Macron akisema ni mahitaji ya kiuchumi kutokana na watu wengi kuwa na umri mkubwa.