Uzbekistan imepiga kura Jumapili juu ya marekebisho ya katiba ambayo yanaahidi raia ulinzi mkubwa wa kijamii kwa mabadilishano ya kuondoa ukomo wa muhula wa Rais Shavkat Mirziyoyev.
Hatua hiyo inaweza kumruhusu rais huyo kugombea mihula miwili zaidi ya miaka saba.
Mirziyoyev, 65, amesifiwa ndani na nje ya nchi kama mwanamageuzi mliberali kwa kuachna na sera za uongozi uliopita za kujitenga na mwelekeo wa serikali kandamizi.
Wakati washirika wa Tashkent wa Magharibi hawana uwezekano wa kuidhinisha jaribio la kuongeza mamlaka ya urais, Uzbekistan ina hatari kidogo kutokana na mataifa ya Magharibi kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa mataifa yote ya zamani ya Umoja wa Soviet katika juhudi zake za kuitenga Russia kutokana na uvamizi wake dhidi ya Ukraine.