Waziri Mkuu Abiy na maafisa wengine walikutana leo na kufanya majadiliano na ujumbe wa TPLF kuhusu maendeleo ya mchakato wa amani, Shirika la Utangazaji la Ethiopia lilisema kwenye akaunti yake ya Twitter.
Matokeo yake , Waziri Mkuu Abiy alipitisha maamuzi kuhusu kuongeza safari za ndege, benki na masuala mengine ambayo yangeongeza uaminifu na kurahisisha maisha ya raia.
Serikali ya Addis Ababa na vikosi vya chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) vilitia saini makubaliano mwezi Novemba kusitisha mapigano kabisa, na kumaliza mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu na mamilioni wengine kupoteza makazi yao.
Mkutano wa Ijumaa ulikuwa wa kwanza wa Abiy na wasimamizi wakuu wa eneo la kaskazini la Tigray tangu mapigano yazuke.