India na China ni miongoni mwa nchi kadhaa zinazoshiriki katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya wiki moja ya Russia yaliyopangwa kuanza Alhamisi mashariki mwa nchi, kulingana na shirika la habari la serikali la Russia Tass.
Wakati India iliwahi kushiriki katika mazoezi ya kijeshi ya kimataifa nchini Russia kikosi cha India kilikuwa sehemu ya mazoezi ya kijeshi ya Zapad yaliyofanyika Septemba 2021 wachambuzi wanasema ushiriki wake katika mazoezi ya kijeshi ya "Vostok-2022" katikati ya uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine unathibitisha uhusiano wa New Delhi wa kirafiki na Moscow licha ya ushirikiano wake wa kimkakati unaoimarika na Marekani.
Kushiriki kwa India katika mazoezi nchini Russia si jambo la kawaida, lakini wakati huu, pia wanajenga hoja ya kisiasa, "alisema Manoj Joshi, mshiriki mashuhuri huko Research Foundation mjini New Delhi . New Delhi inasisitiza kwamba itafuata msimamo huru ambao imechukua kutokana na mzozo wa Ukraine na kuendelea kutoegemea upande wowote kati ya Marekani na Russia.