Ofisi ya rais wa Ukraine imeripoti mapigano makali Jumanne katika mkoa wa Kherson kusini mwa Ukraine, eneo linalokaliwa na vikosi vya Russia ambapo Ukraine inasema imeanzisha mashambulizi ya kujaribu kulichukua tena eneo hilo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliapa katika hotuba yake ya Jumatatu usiku kwamba vikosi vya Ukraine vitalikomboa eneo lao. Alisema Ukraine itavifukuza vikosi vya Russia mpakani.
Ikiwa wanataka kuishi, wakati wakati umefika kwa jeshi la Russia kukimbia. Nendeni nyumbani,” alisema.
Wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema Jumanne kwamba kufikia mapema Jumatatu, "vikosi kadhaa vya Wanajeshi wa Ukraine viliongeza uzito wa milio ya risasi katika sekta za mstari wa mbele kusini mwa Ukraine.