MPLA, kinachoongozwa na João Lourenço tangu mwaka wa 2017, kimetawala nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani Afrika, tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975.
Lakini chama cha upinzani cha muda mrefu cha UNITA, kina nguvu zaidi kuliko hapo awali, huku hasira ikiongezeka kutokana na kushindwa kwa serikali kubadili utajiri mkubwa wa mafuta kuwa hali bora ya maisha kwa wote.
Your browser doesn’t support HTML5
Zaidi ya Waangola milioni 14 wamejiandikisha kama wapiga kura na watamchagua rais na wabunge 220 kwa wakati mmoja, kwa kuweka alama moja kwenye karatasi ya kupigia kura.
Utafiti wa Afrobarometer mwezi Mei ulionyesha idadi ya Waangola wanaopendelea UNITA, inayoongozwa na Adalberto Costa Júnior, imeongezeka hadi 22% kutoka 13% mwaka 2019, bado pointi saba nyuma ya MPLA. Hata hivyo, wakati wa utafiti huo, aribu nusu ya wapiga kura walikuwa hawajaamua.