Miili ya raia 1,150 imepatikana nchini Ukraine katika eneo la Ktiv, tangu Russia ilipoivamia nchi hiyo, na kati ya asilimia 50 mpaka 70 ya miili hiyo ina majeraha ya risasi kutokana na bunduki ndogo ndogo.
Mkuu wa polisi wa Kyiv Andriv Nebytov, amesema kwamba idadi kubwa ya miili hiyo imepatikana katika mji wa Bucha, ambako mamia ya maiti imepatikana tangu wanajeshi wa Russia walipoondoka.
Ukraine imesema kwamba raia waliuawa na wanajeshi wa Russia katika mji wa Bucha.
Hakuna taarifa huru kudhibitisha ripoti hizo au mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa watu hao.
Russia imekanusha madai kwamba wanajeshi wake wamekuwa wakiwalenga raia tangu Februari 24 walipoivamia Ukraine.
Imetaja madai ya mauaji ya raia huko Bucha kuwa habari za uongo zenye lengo la kulichafua jeshi la Russia.