Russia iliongeza muda wa mazoezi Jumapili huko Belarus

Russia yaongeza muda wa mazoezi ya kijeshi Belarus

Russia siku ya Jumapili iliongeza muda wa mazoezi yake ya kijeshi huko Belarus kwenye mpaka wa kaskazini mwa Ukraine baada ya siku mbili za makombora huko mashariki mwa Ukraine kati ya vikosi vinavyotaka kujitenga Russia na vikosi vya Ukraine.

Mazoezi hayo na vikosi vya Belarus yalikuwa yamepangwa kukamilika Jumapili. Yaliongezwa muda kufuatia Rais wa Russia Vladmir Putin kuonyesha nguvu ya vikosi kwenye mpaka wa Ukraine ambako kuna kiasi cha wanajeshi wapatao 150,000 wakiambatana na mazoezi ya wanamaji, huko Black Sea kusini mwa Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alikiambia kipindi cha State of the Union cha CNN kwamba ongezeko la haraka la kupelekwa wanajeshi wa Russia katika wiki za karibuni mashambulizi ya mtandao kwenye wizara ya ulinzi ya Ukraine na mabenki makubwa wiki iliyopita na hivi sasa mlipuko mpya wa mapigano huko mashariki mwa Ukraine ambao uliuwa wanajeshi wawili wa Ukraine unaashiria kwamba Moscow inafuata azma yake kabla ya vita kubwa. Kila kitu kinachobainisha kuelekea kwenye uvamizi tayari kinafanyika, Blinken alisema.