Naye Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guteress amewataka viongozi wa kijeshi kumuachilia huru mara moja rais Roch Marc kabore anaeshikiliwa na wanajeshi pamoja na mawaziri wake.
Wakati huo huo zaidi ya watu 1,000 walikusanyika katika mji mkuu Ouagadougou ili kuonyesha uungaji mkono wao kwa mapinduzi ya kijeshi.
Baraza jipya la utawala lililopewa jina la MPSR linaongozwa na Luteni Kanali Paul Henri Sandaogo Dambia lilifunga mipaka ya nchi, kuweka amri ya kutotoka nje usiku, kusitisha katiba na kuvunja serikali na bunge, na kusema kwamba litairejesha nchi kwenye uongozi wa kikatiba, bila pamoja na hivo kusema lini litafanya hivo.