Dhoruba hiyo ambayo ilianzia mashariki mwa Madagascar ilisababisha mvua kali ambayo imeleta mafuriko na maporomoko ya ardhi katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.
Kulingana na takwim iliyotolewa leo na idara ya majanga ya Madagascar, watu 34 walifariki na wengine 65,000 wamekoseshwa makazi yao tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.
Baada ya kuvuka bahari ya Hindi, mvua kali iliyosababishwa na dhoruba hiyo ilinyesha kaskazini na katikati mwa Msumbiji.
Watu 2 walifariki na 49 kujeruhiwa katika mkoa wa Zambezia, kulingana na idara ya kitaifa ya majanga nchini Msumbiji.
Maafisa wa Serikali ya Msumbiji na mashirika ya Umoja wa mataifa wanakadiria kuwa watu 500,000 waliathiriwa na dhoruba “ Ana” katika mikoa ya Nampula, Zambezia, na Sofala.