Kampuni ya AstraZeneza, imesema kwamba chanjo yake dhidi ya virusi vya Corona, ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virus vya Corona, Omicron.
AstraZeneca imesema kwamba utafiti uliofanywa katika chuo kikuu cha Oxford umebaini kwamba dozi ya tatu ya chanjo ya AstraZeneza inaimarisha kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Omicron.
Utafiri huo ambao haijachapishwa katika jarida la matibabu, unakaribiana na utafiti uliofanywa kuhusu chanjo za Pfizer na Moderna ambao umesema kwamba dozi ya tatu inazuia maambukizi ya Omicron.
Kampuni ya AstraZeneca vile vile imesema kwamba inatengeneza chanjo maalum kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya Omicron.
Wanasayansi na serikali, wanafanya kila juhusi kupata chanjo itakayozuia virusi vya Omicron kuendelea kusambaa kote duniani.
Kusambaa kwa virusi hivyo kumesababisha wasiwasi mkubwa kote duniani wakati huu wa msimu wa krismasi na sherehe za mwaka mpya.