Ndege yaanguka DRC, Watatu wafariki

Ramani ya DRC

Watu watatu wamefariki kufuatia ajali ya ndege iliotokea katikamkoa wa Kivu kusini, mashariki mwa Jamhuri ya kidmeokrasia ya Congo.

Waziri wa uchukuzi wa mkoa huo Alimasi Malumbi amethibitsiha habari hizo.

Ndege hiyo iliyokuwa imebeba watu sita imeanguka umbali wa kilomita 15 kutoka mji wa Shabunda.

Taarifa zaidi kuhusu kampuni inayomiliki ndege hiyo hazijatolewa.

Ajali za ndege mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hutokea kila mara.

Watu 27 walifariki mwaka 2019 baada ya ndege kuanguka katika mji wa Goma wenye idadi kubwa ya watu.