Wazee kupewa zawadi Bulgaria baada ya kupewa chanjo dhidi ya Covid 19

Muuguzi wa afya akiwa ameinama, ishara ya kupumzika, karibu na mgonjwa wa Covid 19 katika chumba ch akuwahudumia wagonjwa mahtuti cha Lozenets Sofia. November 9, 2021.

Serikali ya Bulgaria imetangaza zawadi ya pesa kwa watu wazee watakaokubali kuchomwa chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Waziri mkuu Kiril Petkov, amesema kwamba hatua hiyo ni sehemu ya kuongeza kasi ya watu kupewa chanjo dhidi ya virusi hivyo hatari.

Kulingana na mpango huo, kila mtu mzee nchini Bulgaria, atakayepokea chanjo dhidi ya Corona, atapewa zawadi ya dola 43 kila mwezi kwa mda wa miezi sita.

Watu wazee ambao tayari wamepata chanjo hiyo nao watapewa zawadi hiyo ya pesa.

Asilimia 27 pekee ya watu nchini Bulgaria wamepata chanjo dhidi ya Corona. Nchi hiyo inaongoza kwa idadi ya vifo kutokana na Corona katika umoja wa ulaya.