Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis amewasihi makadinali, askofu na viongozi wa kanisa hilo kuwa wanyenyekevu wakati huu wa msimu wa krismasi.
Papa Francis ametumia ujumbe wake wa krismasi kuwataka viongozi wa Vatican kuwajibika kitabia na mapungufu yao ya kibinafsi.
Amesema kwamba majivuno, e na kukosa kuzingatia maadili ya kanisa hilo vimepeleka kuzorota kwa maisha yao ya kiroho na kuvuruga malengo ya kanisa hilo.
Francis amewakemea viongozi wanaojificha ndani ya utamaduni wa kanisa katoliki badala ya kuwa wanyenyekevu.
Alikuwa akiwahutubia makadinali na maaskofu hao katika ukumbi wa baraka, uliopambwa kwa miti ya krismasi na mapambo mengine ya kuvutia.