Poland na Lithuania wameiunga mkono Ukraine na kutoa mwito kwa mataifa ya magharibi yenye nguvu kuweka vikwazo mara moja dhidi ya Russia kutokana na kuongeza vikosi vyake katika mpaka wa Ukraine.
Wakati hofu ya Russia kuivamia Ukraine ikiongezeka, rais wa Poland, Andrzej Duda, rais wa Lithuania Giyanas Nauseda, na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Jumatatu walitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuharakisha vikwazo dhidi ya Russia kutokana na kuendelea na uchokozi wake dhidi ya Ukraine.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amerejea mwito wake wa kuchukuliwa hatua zaidi za kuizuia, kwa kuweka vikwazo vikali na vigumu ili kuondoa fikra zozote za kukuza mgogoro ambao anaona mpaka sasa vimepuuziwa na Marekani pamoja na wanachama wa NATO wa magharibi mwa Ulaya.
Hata hivyo onyo limetolewa kwa Russia kwamba itakabiliwa na hali ngumu endapo itaivamia Ukraine.