Maandamano yasababisha vifo Goma, DRC

Afisa wa polisi na raia wawili wameuwawa wakati wa maandamano katika mji wa goma mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumatatu, kutokana na kuzorota kwa usalama kwa mujibu wa polisi na asasi ya kiraia.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba mawe makubwa yaliwekwa barabarani ambapo waandamanaji walikusanyika kukabiliana na polisi katika maandamanao ya kupinga ghasia katika eneo hilo, na inaaminika kuwa ni wapinzani wa vikosi vya usalama kutoka katika taifa jirani la Rwanda na kusababisha hali isiyo ya utulivu.

Serekali imekanusha madai kwamba vikosi vya Rwanda vinakwenda kusaidia.

Watu wengi wa Goma wamechoshwa na kuongezeka kwa mashambulizi yanayo fanywa na makundi kadhaa yenye silaha katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri ambayo yamesababisha serekali kutangaza hali ya tahadhari licha ya uwepo wa jeshi na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.