Ikulu ya Afrika kusini Jumatatu imesema rais Cyril Ramaphosa amerejea kazini baada ya kujitenga kwa wiki moja kutokana na kugundulika aliambukizwa virusi vya covid 19.
Ramaphosa ambaye alipewa chanjo ya Johnson and Johnson mwezi Februari, alikutwa na virusi vya covid 19 Disemba 12 na kupatiwa matibabu kwa dalili sizizo kali za ugonjwa huo.
Rais amerudi kazini na ataongoza mkutano wa baraza la mawaziri Jumatano, Ofisi ya rais imesema katika taarifa.
Katika siku chache zilizopita, mlipuko ambao umeikumba nchi nzima uliaminika kuhusishwa na aina mpya ya kirusi cha Omicron uliambukiza zaidi ya watu 20,000 kwa siku, ingawaje idadi ya maambukizi mapya ilishuka mwishoni mwa jumaa.