Utafiti mmoja umeonyesha chanjo ya Covid-19 ya Pfizer-BioNTech inafanyakazi kiasi nchini Afrika Kusini katika kuwalinda watu wasipate maambukizi ya virusi nje ya hospitali toka aina mpya ya virusi Omicron kugunduliwa.
Utafiti huo uliofanyika kiuhalisia na matokeo yake kuchapishwa Jumanne, unaonyesha kati ya Novemba 15 mpaka Desemba 7 watu ambao walikuwa wamepata dozi mbili za chanjo walikuwa na asilimia 70 ya kuwawezesha wasilazwe hospitali ikiwa chini ya asilimia 93 kulingana na takwimu za wimbi la maambukizo ya virusi vya Delta.
Inapokuja suala la kujiepusha maambukizo kwa pamoja utafiti uliofanywa na taasisi ya bima binafsi ya Afrika Kusini, Discovery Health, umeonyesha kwamba ulinzi dhidi ya maambukizi ya Covid-19 umeshuka mpaka asilimia 33 kutoka asilimia 80 ya awali.
Takwimu kutokana na uchambuzi uliofanyika kiuhalisia ni za kwanza kuonyesha namna chanjo zinaweza kufanyakazi dhidi ya virusi vipya vya Omicron nje ya tafiti za kimaabara ambazo mpaka sasa zimeonyesha kupungua uwezo katika kukabiliana na virusi.
Matokeo ya utafiti yalitegemea uchambuzi wa taasisi ya Discovery ya utafiti wa kitabibu na timu za wataalamu wakishirikiana na baraza la utafiti wa kitabibu la Afrika Kusini.
Afrika Kusini iliufahamisha ulimwengu mwezi Novemba uwepo wa virusi vipya ya Omicron, na kutoa ishara kwamba vinaweza kusababisha wimbi lingine la maambukizi duniani, na kusabaisha kuwekwa marufuku za kusafiri kwenda kusini mwa Afrika.
Maambukizi ya Afrika Kusini kwa siku yameongezeka mpaka zaidi ya 20,000, huku asilimia 35 ya vipimo vikirejea na maambukizo katika viambatanisho vya Jumanne na zaidi watu ya 600 wakilazwa na vifo vikiwa 24.