Bobi wine ameandika ujumbe wa twiter, unaoambatana na picha, kuonyesha namna polisi wamepiga kambi nyumbani kwake.
Bobi Wine alikuwa amepanga kumfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha NUP kujaza nafasi ya mwenyekiti wa wilaya.
Rais Yoweri Museveni anatarajiwa wilayani Kaunga kumfanyia kampeni mgombea wa chama kinachotawala cha National resistance movement NRM.
Uchaguzi utafanyika alhamisi wiki hii.
Vyombo vya habari vya Uganda vimeripoti kwamba idadi kubwa ya polisi na wanajeshi wanashika doria wilayani Kayunga wakati kampeni zikiendelea.
Kayunga ilikuwa ngome ya kisiasa ya chama kinachotawala hadi viongozi kadhaa walipochaguliwa kwa tiketi ya chama cha upinzani katika uchaguzi mkuu uliopita.
Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia kifo cha mwenyekiti aliyechaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita.