Umoja wa mataifa Jumatano umewaonya viongozi wa Sudan kusini kwamba mchakato wa amani dhaifu wa taifa hilo changa uko chini ya tishio kubwa kwa kushindwa kupiga hatua ya kuridhisha, ukitoa wito wa haraka wa kufufua mazungumzo.
Taifa hilo lilikumbwa na usalama mdogo wa kila mara tangu lijipatie uhuru mwaka wa 2011, ikiwemo vita vibaya vya miaka mitano vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wanajeshi watiifu kwa rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar, vita ambavyo vilisababisha vifo vya watu 400,000.
Makubaliano ya mwaka wa 2018 ambayo yalimaliza vita yalikwamishwa na mivutano kati ya pande hasimu, na vipengele muhimu vya makubaliano hayo havijatekelezwa.
Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Sudan kusini Nicholas Hayson amesema mchakato huo unaweza kuwa hatarini iwapo utashindwa kushika kasi.
Ameumbia mkutano wa waandishi wa habari kwamba pande zote lazima zichukuwe ari mpya kwenye mchakato huo na kuonyesha nia thabiti ya kisiasa ili kukamilisha masuala nyeti ya makubaliano hayo.
Hayson ametoa pia tahadhari juu ya mzozo mkubwa wa mafuriko nchini humo, ambao uliathiri watu laki 8 kufuatia miezi sita ya mvua kubwa.