Siku za kufanya kazi zapunguzwa UAE

Bendera ya UAE

Umoja wa falme za kiarabu umepunguza siku za kufanya kazi hadi siku nne na nusu.

Wikendi kwa wafanyakazi itakuwa inaanza jumamosi hadi jumapili, badala ya ijumaa hadi jumamosi, ilivokuwa awali.

Wiki ya kazi kitaifa itakuwa ya lazima kwa taasisi zote za serikali kuanzia Jnauari na inalenga kusawazisha shughuli za kikazi na za kibinafsi Pamoja na ushindani wa kiuchumi.

Umoja wa falme za kiarabu ni nchi ya kwanza duniani kuanzisha wiki ya kikazi kitaifa ambayo ni fupi kuliko siku tano za kawaida za kufanya kazi kote duniani.

Nchi hiyo inakuwa nchi pekee ya Ghuba kuwa na wikendi kuanzia jumamosi hadi jumapili, na kuwa sawa na ilivyo katika nchi zingine zisizo za kiarabu.

Wikendi itakuwa ikianza Ijumaa adhuhuri, siku ya maombi kwa waumini wa dini ya kiislamu.