Abiy Ahmed kuongoza mapigano dhidi ya TPLF

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipokuwa anakula kiapo ch akuingia madarakani katika majengo ya bunge mjini Addis Ababa, Ethiopia

Chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali ya Ethiopia Fana leo kimeripoti kwamba waziri mkuu Abiy Ahmed amekwenda kwenye mstari wa mbele wa mapigano ili kuongoza vita dhidi ya wapiganaji wa Tigray, na naibu waziri mkuu Demekele Mekonnen Hassen atasimamia shughuli za kawaida za serikali wakati waziri mkuu hayupo.

Msemaji wa serikali Legesse Tutu ameelezea kukabidhi huko kwa baadhi ya shughuli za serikali za kila siku katika mkutano wa waandishi wa habari, ripoti ya shirika la habari la serikali, Fana imesema.

Jumatatu, Abiy alitangaza kwamba anapanga kuongoza mwenyewe vita dhidi ya wapiganaji wa Tigray na washirika wao.

Kutokana na tangazo hilo inaripotiwa watu wengi wamejiandikisha wiki hii kujiunga na jeshi la taifa linalokabiliwa na matatizo makubwa.

Mwezi uliopita, wanajeshi wa Tigray walitishia kuuvamia mji mkuu Addis Ababa, wamekuwa pia wakipambana vikali kujaribu kufunga njia ya usafirishaji inayounganisha Ethiopia na bandari kubwa katika kanda hiyo ya Djibouti