Feltman, aliwaeleza wanahabari kwa ufupi mjini Washington baada ya kurejea kutoka Ethiopia.
Mwakilishi huyo alirejea Jumatatu, ambapo alikutana na waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, na walijadili uwezekano wa suluhisho la kidiplomasia kumaliza mgogoro uliochukuwa mwaka mzima ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni wengine kukimbia makazi yao katika taifa hilo la pili Afrika kwa idadi kubwa ya watu.
Amesema kwamba pande zote yaani serekali ya waziri mkuu Ahmed, na TPLF wanaona njia pekee ya kupata ushindi ni mapigano ya kijeshi.