Ivory Coast imeongeza uwekezaji eneo la kaskazini mwa nchi kukabiliana na msimamo mkali

Ivory Coast inaongeza kasi katika uwekezaji kwa kujenga shule na kutengeneza ajira katika eneo la kaskazini mwa nchi.

Hatua hiyo ni katika kutoa fursa zaidi na kukabiliana na ghasia za makundi yenye msimamo mkali amesema Waziri mkuu wa taifa hilo Jumatatu.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba kaskazini mwa Ivory Coast ni changamoto kufikiwa na huduma za kibiashara ambako ni kwenye mpaka na Mali na Burkina Faso.

Katika eneo hilo kuna makundi yenye msimamo mkali yanayofanya oparesheni zake na mashambulizi ya kuvuka mpaka yameongezeka.

Matendo ya uandikishwaji kwa vijana wa huko yameongeza wasiwasi ambapo Waziri mkuu Patrick Achi amewaeleza wanahabari na kuongeza kwamba serekali itaongeza ulinzi katika mpaka pamoja na washirika wake kutoka mataifa ya magharibi.

Makundi kama Al Qaeda na Islamic State yameongeza shughuli zake katika eneo la Sahel katika miaka ya hivi karibuni kwa kuandikisha vijana ambao wanakosa fursa za kimaisha.