Nigeria: Matumaini ya kupata walio hai kutoka kwa jengo lililoanguka yafifia

Waokoaji wamebeba maiti kutoka kwa jengo lililoanguka mjini Lagos, Nigeria.

Idadi ya vifo kutokana na kuporomoka kwa jengo lililokuwa linajengwa katika mji wa Lagos nchini Nigeria, imefikia watu 36.

Maafisa wa uokoaji wamekuwa wakitafuta manusura tangu jengi hilo la gorofa 21 lilipoanguka jumatatu lakini hakuna mtu amepatikana akiwa hai.

Familia za waliokuwa kwenye jengo hilo wameeleza kukasirishwa na namna shughuli ya uokoaji inavyoendeshwa, wakisema wanaofanya kazi hiyo wanafanya kwa kuzembea sana na ni kama hawatafuti manusura.

Gavana wa jimbo la Lagoa amesema kwamba shughuli ya uokoaji inaendelea na kwamba tume huru imeundwa kuchunguza kilichopelekea jengo hilo kuanguka.