DRC: Jeshi laongezewa mda kudhibithi Kivu na Ituri

Wanajeshi wa DRC wakipiga doria

Baraza la senate la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo limeongeza mda wa jeshi kudhibithi mikoa ya Kivu kaskazini na Ituri kwa mara ya 11 katika juhudi za kurejesha usalama mashariki kwa nchi hiyo.

Waziri wa haki Rose Mutombo ameasilisha mswada katika senate na kueleza juhudi zinazochukuliwa na jeshi kurejesha hali ya utulivu katika sehemu hizo.

Spika wa senate amenukuliwa akisema kwamba maseneta 89 wameshsiriki katika kupiga kura, na 84 wameidhinisha mswada huo.