Mtihani mkubwa kwa ANC katika uchaguzi wa serikali za mitaa

Rais wa Afrika kusini na kiongozi wa chama cha ANC Cyril Ramaphosa

Wapiga kura nchini Afrika wanashiriki katika awamu ya sita ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa tangu mwaka 1994 wakati utawala wa wazungu ulipomalizika.

Wapiga kura wanawachagua meya na madiwani wa wilaya watakaokuwa na jukumu la kusimamia utoaji wa huduma muhimu kama maji, usafi mijini, umeme na kukarabati barabara.

Hata hivyo, idadi ya wapiga kura ni ndogo.

Tume huru ya uchaguzi imesema kwamba theluthi tatu ya watu ambao wamefikisha umri wa kupiga kura hawajajisajili kupiga kura.

Zaidi ya vyama 320 vya siasa vinashiriki uchaguzi wa leo.

Chama kinachotawala cha African national congress ANC, kinakabiliwa na ushindani mkali kutokana na madai ya ufisadi na migawanyiko kati ya viongozi wake.

Chama kikuu cha upinzani cha democratic alliance kinatarajia kuongeza idadi ya wawakilishi