Taasisi ya kitaifa inayosimamia Mafuta nchini Msumbiji, inatarajiwa kutangaza zabuni kwa kampuni mpya za kuchimba mafuta na gesi mwezi ujao.
Shughuli hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi March 2022.
Jumla ya vitalu 16 vya kuchimba mafuta vinatarajiwa kupata wachimbaji.
Vitano vipo Rovuma karibu na Tanzania, saba katika sehemu ya Angoche pwani ya Nampula, viwili katika sehemu ya Zambezi na viwili vipo mto Save.
Taasisi ya mafuta ya Msumbiji inalenga kuongeza kuongeza kiwango cha madini ahydrocarbon anayotumika kutengeneza umeme, mbolea na mafuta.
Kampuni kubwa ya kuchimba mafuta ya Ufaransa Total, inachimba kiasi kikubwa cha gesi kaskazini mwa msumbiji.
Total imeekeza kiasi cha dola bilioni 20, ikiwa ndio uwekezaji mkubwa zaidi Afrika.