Jeshi na waandamanaji wapambana Sudan

Vikosi vya usalama Alhamisi, vilipambana na waandamanaji waliokuwa na hasira wakipinga mapinduzi ambayo yamezidi kuzorotesha kipindi cha mpito cha kidemokrasia, na kisababisha ukosolewaji mkubwa kimataifa.

Takriban waandamanaji wanne wameuwawa kwa mujibu wa maafisa wa afya katika siku ya nne mfululizo ambapo ghasia zinaendelea mitaani katika jiji la Khartoum.

Hatua hiyo inafanya idadi ya waandamanaji waliouwawa toka Jumatatu yalipotokea mapinduzi kufikia 7 kwa mujibu wa taarifa zilizo tolewa na maafisa wa afya, ambapo watu 170 wameuwawa.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na rais wa Marekani Joe Biden, Alhamisi walititoa mwito wa kurejeshwa kwa serekali ya kiraia ambayo imepinduliwa na jeshi siku ya Jumatatu.

Baraza la usalama limepiga kura zote za ndio kupitisha taarifa inayoelezea kuwa na wasiwasi mkubwa wa hali ya mambo nchini Sudan.