Bei ya mafuta yashuka, mazungumzo kuhusu silaha za nuclear za Iran kuanza

Kiwanda cha mafuta nchini Iran

Bei ya mafuta imeshuka kwa kiwango cha chini kabisa katika mda wa wiki mbili baada ya Iran kusema kwamba mazungumzo na nchi zenye nguvu duniani kuhusu mpango wake wa kutengeneza silaha za nuclear yataanza tena mwishoni mwa mwezi Novemba.

Bei ya pipa la mafuta ghafi imeshuka kwa dola 1.07 na kuuzwa dola 83.51.

Mwakilishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ya nuclear Ali Bagheri Kani, amesema kwamba mazungumzo kati ya Iran na nchi sita zenye nguvu duniani kujaribu kufufua mkataba wa mwaka 2015 wa nuclear, yataanza mwishoni mwa mwezi Novemba.

Makubaliano yanaweza kutoa fursa ya kuondoa vikwazo vikali vilivyowekwa na aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump, dhidi ya Iran, kuhusu mauzo ya mafuta ya Iran, mwaka 2018.

Akiba ya mafuta ghafi imeongezeka kwa kiasi cha pipa milioni 4.3 wiki iliyopita, ikiwa ni mara mbili zaidi.