Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Ned Price, amesema Marekani inataka kuona serekali ya mpito inayoongozwa kiraia inarejea mara moja, na kufuatwa kwa matakwa ya raia.
Amesema kwamba msaada huo uliositishwa wa dola milioni 700, ulilenga kusaidia uchumi wa taifa hilo, na kufanikisha kipindi cha mpito cha kidemokrasia baada ya kuondolewa madarakani Omar al Bashir miaka miwili iliyopita.
Pia msemaji huyo wa wizara amelionya jeshi kutofanya udhalimu wowote kwa waandamanaji baada ya kutokea taarifa kwamba watu watatu wameuwawa katika oparesheni za kusaka waandamanaji wanaopinga hatua ya jeshi kuchukuwa utawala.
Jenerali wa juu wa Sudan, Abdul Fattah al-Burhan, kwenye hotuba ya televisheni alisema jeshi limezunguka nyumba ya kiongozi wa mpito wa Sudan.