Wanamgambo wauwa watu 10 Niger

Wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wenye msimamo mkali wamewauwa wanakijiji 10 katika shambulizi la msikitini mapema wiki hii magharibi mwa Niger.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Tillaberi kwa mujibu wa taarifa za wakazi wa eneo za Jumatano.

Shambulizi la Jumatatu lilifanyika katika Kijiji cha Abankor katika eneo la mpaka unaokutanisha mataifa matatu ya Niger, Mali na Burkina Faso.

Afisa wa mji wa Banibangou ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba washambuliaji hao waliwasili wakiwa katika pikipiki wakati wa sala ya jioni, na walio uwawa walikuwa ndani ha msikiti.

Mkazi wa mji wa karibu wa Tondiwindi alithibitisha kutokea kwa shambulizi hilo na idadi ya vifo.

Moja ya kituo cha redio katika meneo hayo kimetangaza zaidi ya watu 10 waliouwawa na kuongeza kwamba shambulizi lilitokea mapema jioni.