Marekani yapongeza uchaguzi wa Iraq

Ikulu ya Marekani imetoa pongezi kwa serekali ya Iraq kwa kufanikiwa kufanya uchaguzi Jumanne,kwa amani huku matokeo ya uchaguzi yakisubiriwa.

Msemaji wa White House, Jen Psaki, amesema kwamba Marekani inatoa pongezi kwa serekali ya Iraq kwa kutimiza ahadi yake ya kufanya uchaguzi mapema.

Amesema pindi tu matokeo yatakapo tangazwa, Marekani inatarajia kwamba baraja jipya la uwakilishi litaanza na wawakilishi wataunda serekali itakayo akisi matakwa ya watu wa Iraq.

Chama cha kiongozi wa kidini Muqtada al-Sadr kilikuwa chama kilichopaga kura nyingi za bunge la Iraq kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa awali wa Jumatatu.