Polisi wa Bangladesh wamekamata wakimbizi wa Rohingya takriban 16 katika mfululizo wa uvamizi kwenye kambi zao mjini Dhaka.
Hii ni baada ya mauaji ya kiongozi wa jumuiya ya Wa-Rohingya wiki iliyopita kwa mujibu wa taarifa za mafiasa jana jumapili.
Mtetezi wa haki za binadamu Mohib Ullah, alishambuliwa siku 10 zilizopita na watu wasio julikana nje ya ofisi yake iliyokuwa katika makazi makubwa ya wakimbizi katika eneo la kusini mashariki mwa Bangladesh.
Familia yake, na viongozi wengine wa jumuiya wanashutumu jeshi la wokovu la Arakan Rohingya ARSA kuhusika na mfululizo wa mashambulizi ya vituo vya Myanmar.
Wanasema umaarufu wa Mohib Ullah umelikasirisha kundi hilo, lakini ARSA yenyewe inapinga shutuma hizo za kuhusika na mauji hayo.
Kiongozi huyo aliyekuwa na miaka 48, alikuwa ni Sauti ya utetezi wa Wa-Rohingya 800,000 ambao walikimbia Myanmar.