Rais wa Israel, Reuven Rivlin, Jumatano amesema atawasiliana na vyama 13 vyenye uwakilishi ndani ya bunge kujadili mchakato wa kuunda serekali.
Rais Rivlin, anachukuwa hatua hiyo baada ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu, kushindwa kutimiza hayo baada ya kufika muda uliopangwa wa siku ya Jumanne kuunda serekali mpya ya mesto.
Katika siku zijazo rais Rivlin, anatarajiwa kumpatia fursa nyingine mpinzani wa waziri mkuu Netanyahu, ya kuundwa kwa serekali ya pamoja.
Pia rais huyo ataliomba bunge kuchagua mmoja kati ya wabunge wake kuwa waziri mkuu wa Israel.
Jumbo hilo likitokea wa chama cha Netanyahu, Likud kitakuwa chama cha upinzani hii ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kupita kipindi cha miaka 12.