Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amesema yuko tayari kufanya mashauriano na wadau katika mzozo wa kisiasa wa Somalia ili kupata suluhisho.
Mohamed, aliyefahamika kwa jina la utani Farmaajo, alitoa tangazo hilo Jumapili usiku wakati wa ziara ya kushtukiza mjini Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo alikutana na Rais Felix Tshisekedi, mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU).
Kupitia Wizara yake ya Mambo ya nje, Farmaajo alisema serikali ya shirikisho ya Somalia inaukaribisha Umoja wa Afrika kuwezesha mazungumzo hayo.