Mataifa tajiri yatakiwa kuchangia chanjo zao za ziada

Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa mataifa, taasisi za kifedha, na wanao husika na chanjo, Alhamisi wametoa mwito kwenda kwa nchi tajiri kuchangia chanjo za Covid-19.

Wamesihi chanjo zao zaidi kuzisambaza katika mataifa yenye kipato cha chini ikiwa ni juhudi za kumaliza janga la corona na kurejesha uchumi wa dunia.

Katika hafla iliyo andaliwa na taasisi ya GaviVaccine Alliance kuongeza msaada kwa mradi wa COVAX ambao unatoa chanjo, maafisa hao wamesihi kupatikana kwa kiasi cha dola bilioni mbili ifikapo mwezi Juni.

Fedha ni kwa ajili ya mpango huo wenye lengo la kununua mpaka dozi bilioni 1.8 katika mwaka huu wa 2021.

COVAX imeshasambaza zaidi ya chanjo bilioni 38 katika mataifa 111 katika kipindi cha miaka saba nyingi ya hizo zikiwa za AstraZeneca.