Mkurugenzi wa shirika la biashara la dunia (WTO) amesema Jumatatu kwamba mkutano utafanyika wiki hii wa kushughulikia kutokuwepo kwa usawa katika chanjo ya Covid-19.
Mkutano huo utahudhuriwa na watengenezaji wakubwa wa chanjo, na kushughulikia suluhisho ikiwemo kutumia viwanda ambavyo havijatumiwa vya Africa na Asia.
Mkurugenzi wa WTO, Dr Ngozi Okonjo-Iweala, ameapa kushughulikia masuala katika mtindo tofauti, na kusisitiza kwamba kipaumbele chake ni kushughulikia janga la Covid-19.
Mkutano huo wa Aprili 14 utawakutanisha watengenezaji wa chanjo kutoka Marekani, China, na Russia, ambao utawajumuisha mawaziri kutoka mataifa tajiri na yaliyo endelea, maafisa wa kibenki na kujadili kuhusu usimamizi wa chanjo, kuongeza uzalishaji, na kuondolewa kwa haki za ubunifu wa chanjo ya Covid-19.